Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA MZEE BAN KI MOON ATAKA HARAKA IWEZEKANAVYO MAUWAJI YA WAISLAM YAKOMESHWE C.A.R

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA MZEE BAN KI MOON ATAKA HARAKA IWEZEKANAVYO MAUWAJI YA WAISLAM YAKOMESHWE C.A.R

Written By Unknown on Saturday, 15 February 2014 | Saturday, February 15, 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kukomesha machafuko yanayoendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati. Akizungumza mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon amesisitiza kuwa, jamii ya kimataifa inapasa kuchukua hatua za haraka za kuzuia wimbi la jinai mpya na maangamizi makubwa ya kidini na kikabila nchini humo. Ban Ki moon amesisitiza na hapa tunamnukuu: 'wingu zito jeusi la jinai kubwa na maangamizi ya kidini na kikabila limetanda katika anga ya Afrika ya Kati', mwisho wa kunukuu. Ban Ki moon ameongeza kuwa, iwapo mgogoro wa hivi sasa unaoendelea kutokota Jamhuri ya Afrika ya Kati hautakomeshwa, bila shaka kuna wasiwasi nchi hiyo itaendelea kushuhudia mapigano hadi miongo kadhaa ijayo. Hivi karibuni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International lilikosoa kimya cha jamii ya kimataifa kuhusiana na mauaji yanayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa ya shirika hilo la kimataifa ilieleza kuwa, lina ushahidi wa kutosha unaoonyesha ukatili na mauaji yanayofanywa na kundi la Kikristo la Anti Balaka dhidi ya maelfu ya Waislamu nchini humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi