Ripoti ya umoja wa mataifa imeonya kuwa silaha
zilizokuwa zikipelekwa kwa vikosi vya serikali ya Somali zimeingia
katika mikono ya kundi la Al-shabaab kutokana na ukiukwaji wa utaratibu
katika serikali.
Uchunguzi huo uliofanywa na wataalam walio huru
umesema kuwa silaha za kudungua ndege,mabomu na risasi zilizotoka nchini
Uganda na Djibout haziwezi kuwajibikiwa.Ripoti hiyo sasa inataka taifa la Somali kuwekewa vikwazo vya silaha ambavyo viliondolewa mwaka uliopita.
Wataalam hao wamesema kuwa wana ushahidi kwamba mshauri mkuu wa rais nchini Somali amekuwa akihusika na mpango wa kuwapelekea silaha wapiganaji wa Alshabaab.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!