Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » HATIMAYE AT NA MGANGA WAKE WAKAA KWENYE MEZA BAADA YAKUWA NA UVUMII KUWA AT AMEMKWEPA MGANGA HUYO NA DENI LAKE

HATIMAYE AT NA MGANGA WAKE WAKAA KWENYE MEZA BAADA YAKUWA NA UVUMII KUWA AT AMEMKWEPA MGANGA HUYO NA DENI LAKE

Written By Unknown on Thursday, 13 February 2014 | Thursday, February 13, 2014

Wiki iliyopita, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shariff, alijitokeza na kukiambia kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm kuwa yeye ni mganga wa AT aliyemfanyia manyanga na kumpandisha hadi hapo alipofika, na kwamba kwa sasa msanii huyo amemtelekeza na kumuacha na deni la nyumba la shilingi laki tisa.
Mtu huyo alienda mbali na kudai kuwa, kwa kuwa kazi hiyo ilikuwa siri na aliifanya kuanzia mwaka 2010, mwimbaji huyo wa ‘Nipigie’ alikuwa anaenda nyumbani kwake mara kwa mara usiku, lakini siku moja alienda mchana akiwa amevaa hijabu kuficha sura yake ili asionekane.
AT naye alipoulizwa, alimkana mtu huyo kuwa hamfahamu kabisa licha ya kutajiwa baadhi ya vielelezo alivyovitaja mtu huyo, ambaye alidai pia kuwa na pete, memory card na fimbo ya AT alivyovisau nyumbani kwake.
Hata hivyo, mganga huyo aliamua kuchukua uamuzi na kumripoti kwa mjumbe na hatimaye polisi, kwa hiyo hivi sasa kesi hiyo iko polisi na inaweza kupelekwa mahakamani endapo itakidhi vigezo vya kufikishwa huko.
Watangazaji wa kituo hicho waliweza kuwakutanisha AT na mtu huyo kwenye kipindi ili waweze kufahamu kiundani ‘kipi ni kipi’ na kila mmoja aeleze yake.
Mambo yalienda vizuri huku kila mmoja akijaribu kutoa vielelezo vyake kuonesha kuwa alichokisema ni ukweli kabisa.
Nani mkweli, Shariff ambaye anadai kuwa mganga mwaminifu wa AT aliyetelekezwa, ama AT alimkana na kudai kuwa inawezekana kabisa kuwa amepandikizwa ili kumchafulia jina, na kwamba anatafuta KiCK mjini.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi