Arsenal
inaikaribisha Manchester United katika mchezo ambao ni muhimu kwa timu
zote mbili.Mechi hii kawaida ni mechi inavuta hisia za mashabiki wengi
duniani bila kujali vilabu vipo kwenye hali gani lakini ukifikiria
matokeo ya wikiendi iliyopita, mchezo huu unazidi kuwa muhimu zaidi.
Arsenal
wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kipigo kitakatifu
cha 5-1 kutoka kwa Liverpool jumamosi iliyopita. Majogoo wa jiji
waliipiga Arsenal 4-0 ndani ya dakika 20 tu, kitu ambacho itabidi
Gunners wakiwekee umakini ili wasikutane nacho katika mchezo wa leo.Huku
mbio za ubingwa zikiwa zimepamba moto, Arsenal leo wanahitaji kushinda
ili warudi kileleni vinginevyo wanaweza kujikuta wakizidi kuteremka
chini kwenye msimamo. Matokeo ya wiki hii hayakuwa mazuri kabisa
ukizingatia ratiba ngumu waliyonayo. Baada ya kucheza na United leo,
Arsenal watakutana tena Liverpool lakini safari hii kwenye FA Cup, baada
ya hapo watacheza na Bayern Munich katika Champions League.
Man
Utd kwa upande mwingine wapo katika nafasi ya saba, wakitoka kutoka
sare ya 2-2 na Fulham wanaoshika nafasi ya mwisho kwenye ligi. Ilikuwa
ni mechi ambayo United ilishambulia sana, lakini wakakosa makali kwenye
lango la wapinzani na mwishoni wakaonjeshwa utamu wa dawa yao wenyewe
kwa kuruhusu bao la dakika ya mwisho kabisa ya mchezo na kupoteza pointi
mbili muhimu. Huku matumaini yao ya kucheza Champions League yakianza
kupotea, matokeo ya wikiendi yaliwafanya kuwa nyuma kwa pointi tisa
kutoka kwa wanaoshika nafasi ya nne Liverpool, ambao pia wana wastani
mkubwa wa mabao. United watakuwa na matumaini ya kurudisha utamaduni wao
wakati Sir Alex Ferguson alipokuwa kocha, huku wakiomba timu nyingine
zinazogombea nafasi ya nne za juu zipatae matokeo mabaya.
Mechi
ya Arsenal vs Man Utd siku zote imekuwa na upinzani mkubwa kuanzia
miaka ya mwanzoni miaka ya 2000. Timu hizi mbili zimekuwa zikigombea
ubingwa zenyewe kwa zenyewe na upinzani wao ulikuwa ukionekana wakati wa
mechi zao. Enzi za ugomvi wa Viera na Roy Keanezimepita lakini upinzani
bado upo. Huku usajili wa Van Persie kutoka Arsenal kwenda Old
Trafford, imezidisha uhasama miongoni mwa mashabiki, hasa zaidi baada ya
Van Persie kufunga mara kadhaa dhidi ya Arsenal tangu ajiunge na
United, likiwemo bao la ushindi katika raundi ya kwanza.
Habari za Timu
Arsenal
Arsenal
walikosa ubunifu na walikuwa wepesi kwenye kiungo siku ya jumamosi huku
pengo la Flamini likionekana wazi. Kiungo huyo wa kifaransa anatumikia
adhabu ya mechi 3 hivyo kwa mara nyingine atakosekana kwenye mchezo wa
leo. Mchezaji mpya Kim Kallstrom ni majeruhi kama ilivyo kwa Walcott na
Diaby. Vermaelen anakaribia kurejea lakini sio rahisi kucheza kwenye
mchezo huu, Ramsey atakuwa nje mpaka mwezi ujao. Wenger anategemewa
kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza huku Gibbs, Rosicky NA
Podolski wote wakitegemewa kuanza.
Man United
Phil
Jones anaweza kurudi kwenye kikosi cha kwanza cha United mara baada ya
kurudi kutoka kwenye majeruhi. Fellaini, Nani na Ferdinand wote watakuwa
nje kwa pamoja na Cleverley na Evans ambao walipata majeruhi hivi
karibuni.
Vikosi vinavyoweza kuanza
Takwimu mbalimbali za kuvutia
- Gunners wameshinda mechi zao sita kati ya nane zilizopita za Barclays Premier League walizocheza nyumbani kwa mabao 2-0.
- Arsenal wameshinda mechi moja tu kati ya 10 za premier league dhidi ya Arsenal (W1 D2 L7).
- Hii ni mara ya kwanza Arsenal na Manchester United zinakutana kwenye Premier League baada ya kushindwa kushinda kwenye zao za nyuma tangu April 2008.
- Arsenal wameweza kuwa na clean sheets 10 katika mechi 11 zilizopita katika mashindano yote ndani ya dimba la Emirates.
- Robin van Persie amefunga katika mechi 5 zilizopita za premier league baina ya timu hizi mbili - mabao 3 kwa United - mabao mawili kwa Arsenal.
- Wayne
Rooney amefunga mabao 10 ya premier league dhidi ya Arsenal. ndio
mchezaji anayeongoza kufunga mabao mengi katika historia ya timu hizo
mbili.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!