Falcao alipo tembelewa na Rais wa Cololombia Hospitalini nchini Ureno |
Falcao ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi
Kuu Ufaransa, ligi ambayo imevamiwa na matajiri wa Russia na Qatar
wanaomwaga pesa za kutosha katika klabu mbili za Paris Saint Germain
(PSG) na Monaco.
Staa huyo wa kimataifa wa Colombia anayekipiga
Monaco akiwa ametokea Atletico Madrid mwanzoni mwa msimu huu amempita
kwa pesa hata nyota mwenye maringo wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic.
Falcao anapokea kiasi cha Euro 1.2 milioni kwa
mwezi baada ya makato ya kodi wakati, Ibra anapokea kiasi cha Euro
800,000 kwa mwezi baada ya makato ya kodi. Kiasi hiki cha Ibra ni baada
ya kuongezewa mshahara Septemba mwaka jana. Mishahara halisi ya
wachezaji wote inaongezewa na bonasi zao pamoja na mikataba yao binafsi
ya kibiashara.
Anayefuata katika nafasi ya tatu ni mlinzi na
nahodha wa PSG na Brazil, Thiago Silva anayepokea kiasi cha Euro 628,000
kwa mwezi baada ya makato ya kodi huku akifuatiwa na nyota wa kimataifa
wa Uruguay, Edinson Cavani anayekipiga naye PSG.
Nyota huyo wa Uruguay ndiye mchezaji ghali zaidi
katika historia ya soka la Ufaransa akiwa amenunuliwa kwa kiasi cha Euro
65 milioni kutoka Napoli katika kipindi cha majira ya joto kilichopita.
Cavani anaingiza kiasi cha Euro 478,000 kwa mwezi.
Mastaa wawili wa Monaco walionunuliwa kutoka
Ureno, James RodrÃguez na Joao Moutinho wanashika nafasi ya sita na ya
saba. Wakati Rodriguez analipwa kiasi cha Euro 370,000 kwa mwezi,
Moutinho anachukua 342,000.
Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina,
Ezequiel Lavezzi anayekipiga PSG anapokea kiasi cha Euro 329,000 kwa
mwezi huku akishika nafasi ya nane.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!