Balozi wa Marekani nchini Sudani Joseph D Stafford amelazimishwa kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake mara baada ya kusilimu, vimeripoti vyombo vya habari vya ndani vya Sudan.
Pamoja na viongozi wa dini |
katika hadhara ya dini |
Akiitikia Dua |
Stafford baada ya kujiuzulu alichapisha makala katika Sudan Tribune na kusema, "Mimi na mke wangu tumekuwa na bahati sana ya kukutana na watu wengi wazuri (ajabu) katika Sudan ambao wana hamu kubwa na nia ya kuboresha jamii zao".
"Daima tutawakumbuka nyinyi na nchi yenu yenye kuvutia, najua mtaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya maisha bora kama msemavyo 'Fi Kulu Harakah Baraka' (katika kila kujishughulisha kuna baraka)".
Marekani ilimteua Joseph D Stafford kuwa balozi wake nchini Sudan tangu mwaka 1998. Aliwahi kuwa Balozi katika nchi za Nigeria na Gambia.
Miji aliyowahi kufanya kazi ni Baghdad (iraq), Abidjan (ivory coast),Tunis (Tunisia), Algiers (Algeria), na Nouakchott. kuwait,Cairo (Misri), Palermo (italy) na Tehran(Iran).
Stafford anayemudu lugha za kiarabu, kifaransa na kiitaliano alijiunga na wizara ya mambo ya nje ya marekani tangu mwaka 1978. Ana mke na mtoto mmoja.
Ubalozi wa Marekani mpaka sasa haujatoa kauli yoyote kuthibitisha au kukataa habari za Joseph Stafford.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!