Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, jeshi Jekundu la Shirikisho la
Urusi ya Zamani lililazimika kuondoka nchini Afghanistan baada ya
kuikalia kwa mabavu nchi hiyo kwa miaka kumi. Majeshi hayo yaliondoka
baada ya kushindwa kukabiliana na muqawama wa mujahidina wa Kiislamu.
Lengo la Umoja wa Sovieti la kuivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan
mwaka 1979, lilikuwa ni kuizatiti serikali kibaraka ya Kabul iliyokuwa
ikiungwa mkono na Moscow na kueneza satua yake kuelekea maeneo ya kusini
mwa Asia. Hatua hiyo iliyopelekea maslahi ya Marekani kuwa hatarini,
ilikabiliwa na radiamali kali ya Washington sambamba na hatua ya White
House ya kuanzisha operesheni za kuyatoa majeshi ya Umoja wa Sovieti
huko Afghanistan. Hatimaye baada ya miaka 10 wananchi wa Afghanistan
wakisaidiwa na Mujahidina walifanikiwa kuhitimisha uvamizi huo na
kuyatoa majeshi ya Urusi katika ardhi yao.
****
Miaka 232 iliyopita vilianza vita vya majini kati ya Ufaransa na
Uingereza katika pwani ya India. Vita hivyo vilivyodumu kwa muda wa
miezi saba, vilikuwa ni mlolongo wa vita kati ya nchi mbili hizo
vilivyokuwa na lengo la kuikoloni India na kupora utajiri wake.
Ijapokuwa Ufaransa ilishinda vita hivyo, lakini nchi hiyo haikuweza
kurejea India na kuikoloni nchi hiyo, na badala yake Uingereza ilibaki
na kuendelea kuwa mkoloni mkuu huko bara Hindi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!