Siku kama ya leo
miaka 49 iliyopita nchi ya Gambia ilifanikiwa kupata uhuru kutoka kwa
mkoloni Mwingereza na siku kama ya leo hujulikana nchini humo kama siku
ya kitaifa. Gambia ilikuwa koloni la kwanza la Uingereza barani Afrika.
Uingereza iliikoloni nchi hiyo tangu mwaka 1588 na kuendelea kupora
maliasili ya nchi hiyo kwa karibu karne nne. Mwaka 1963 Uingereza ambayo
ilidhoofika kisiasa na kiuchumi kutokana na athari za Vita vya Pili vya
Dunia haikuwa tena na uwezo wa kuendelelea kuikoloni Gambia na nchi
hiyo ikapata utawala wa ndani. Mwaka 1965 katika siku kama ya leo Gambia
ikajipatia uhuru wake.
Siku kama ya leo miaka 180 iliyopita sawa na tarehe 18 Februari mwaka 1834 vikosi vya majeshi ya Ufaransa ambavyo tangu mwaka 1830 vilianza kuikalia kwa mabavu Algeria vilishindwa vibaya na wapiganaji wa Amir Abdulqadir Al Jazairi. Kushindwa huko kulipelekea theluthi moja ya askari wa Ufaransa kuuawa na nusu ya waliobakia kukamatwa mateka. Baada ya Wafaransa kushindwa vibaya kwa mara ya kwanza barani Afrika, nchi hiyo ililazimika kusalimu amri na kuomba yafanyike makubaliano ya amani lakini Amir Abdulqadir Jazairi alikataa ombi hilo hadi baada ya miaka miwili iliyofuata, ambapo alifanikiwa kukomboa karibu ardhi yote ya Algeria kutoka katika mikono ya Wafaransa.
Na tarehe 18 Rabiuthani katika siku kama ya leo miaka 833 iliyopita alizaliwa al Muhaqiq al Hilli, ambaye alikuwa mwanazuoni mkubwa wa fiqhi wa Kiislamu katika mji wa Hilla nchini Iraq. Muhaqqiq al Hilli alikuwa hodari sana katika masuala ya sheria na alibobea pia katika fasihi na uandishi wa mashairi. Baada ya kukamilisha masomo ya awali na kukwea daraja za juu za kiroho na kielimu, alitambuliwa kuwa miongoni mwa wanazuoni mashuhuri wa zama zake. Kitabu muhimu zaidi cha al Muhaqqiq al Hilli ni Sharaiul Islam. Mwanazuoni huyo pia ameandika vitabu vya Nafi', Maarij na al Tanbih. Muhaqqiq al Hilli alifariki dunia mwaka 676 Hijria akiwa na umri wa miaka 74

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!