Katika mechi nyingine za mtoano, Bayer Leverkusen
itakuwa nyumbani kuwakaribisha matajiri wa Ufaransa, Paris
Saint-Germain, wakati AC Milan itajitupa San Siro kucheza na
Wahispaniola, Atletico Madrid.
Barcelona itakwenda Etihad ikiwa kwenye kiwango
bora kabisa, lakini wenyeji wao wakiwa na staa wao, Yaya Toure,
aliyewahi kucheza kwenye kikosi cha Wacatalunya hao kabla ya kutua
England, aliyeapa kufanya kweli uwanjani huku akiwa na lengo la kuivusha
Manchester City kwenye hatua hiyo ya mtoano kwa mara ya kwanza.
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini,
anaamini mastaa wake wawili, Fernandinho na Sergio Aguero, watakuwa fiti
kuwakabili Barcelona, ambapo kocha wake, Gerardo Martino, ana uhakika
wa kupata huduma safi kutoka kwa nyota Lionel Messi na Neymar.
Mchezo huo unatazamwa kama vita ya Kilatino,
kutokana na makocha hao na wachezaji waliotajwa wote kutoka Amerika
Kusini. Barcelona ina uhakika zaidi wa nyota wake kutokana na wengi wao
kuwa fiti, tofauti na Manchester City inayoandamwa na majeruhi.
Kwenye Uwanja wa Emirates, patakuwa hapatoshi;
Arsenal itashuka hapo ikitaka kulipa kisasi dhidi ya Bayern Munich,
ambayo msimu uliopita iliibuka na ushindi uwanjani hapo kabla ya wao
kwenda kupoteza Allianz Arena.
Kocha Arsene Wenger ataingiza uwanjani timu yake
akiwa na uhakika baada ya juzi Jumapili kuichapa Liverpool mabao 2-1
kwenye Kombe la FA na atataka pia kuwamaliza Wajerumani hao.
Lakini, Bayern Munich ikiwa chini ya kocha, Pep
Guardiola, inaonekana kuwa kwenye ubora mkubwa zaidi kutokana na
mwenendo wake kwenye Ligi Kuu Ujerumani ikiongoza kwa tofauti ya pointi
16. Katika kuonyesha kwamba wanajiamini kupita kiasi, mabingwa hao wa
Ulaya watafanya mazoezi yao ya mwisho Ujerumani na kisha watapanda ndege
moja kwa moja kwenda kuivaa Arsenal.
Mechi nyingine za hatua hiyo ya mtoano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya zitaendelea wiki ijayo, wakati Olimpiakos itakapokipiga
na Manchester United, FC Schalke 04 dhidi ya Real Madrid, Zenit St
Petersburg na Borussia Dortmund na Galatasaray watakuwa wenyeji wa
Chelsea.
Katika mchezo huo utakaofanyika Uturuki, Chelsea
itakumbana na straika wake wa zamani, Didier Drogba, ambaye amekuwa moto
zaidi kwenye kikosi hicho cha miaka ya Uturuki.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!