Ukiwa nje ya nchi naimani uko kama mwenye upo gerezani ni mfano wa kipofu asie ona wala kusikia.Issa Jamal Yoya moja wa wanamuziki wa Burundi wenye elimu ya juu na mwenye sasa maisha yake anayapeleka powa.Yoya ukilinganisha na gari analo limiliki lenye takribani milioni kumi nambili na zaidi likiwa ni jipya kutoka Japan au sehemu zingine,lakini Star huyu hajawai ingia mgogoro na chombo cha habari au kuingia mgogoro na mwanamuziki mwenzie au rapa na hadi ifikie kumpelekea aimbe wimbo wakuwachafuwa wenzie kwake haijawai tokea na kwa mujibu wake haitokufa inatokea huyo ni Yoya,tumuache.
Tumchukuwe mwanamuziki Jean Pierre Nimbona alimaarufu kama Kidumu huyu jamaa Kidumu ni famous sana ni tajiri anamaisha marefu sana gharama zake na bajeti zake inawezekana kuwa anawazidi baadhi ya watu wakuu serikalini mfano kama wabunge kwa mujibu wa wachambuzi,ila huyu jamaa hajawai ingia mgogoro na msanii mwenzie wala rapa yeyote hadi eti impelekee kuwatusi wenzie wananuka vikwapa wakapige mswakii....nakadhalika.Kidumu aliwai ingia mgogoro mdogo na Producer Hermy B wa B-Hits lakini mgogoro huwo haukuweza kuchelewa kumalizika na mambo yakawa powa.
Hawo wametajwa hapo ni watu maarufu sana.
Hali imekuwa gumzo sasa hadi mvutano utoke kwenye midomo ya watu uhame redioni na sasa umehamia kwenye mitandao ya kijamii.
Mvutano huwo umekuja baada ya mwanamuziki local artist kutoka hapa nchini Burundi Mugani Desire alimaarufu kama Burundiano mzaliwa wa mkowani Makamba kutowa wimbo ambao mwanzo mwisho wa wimbo huwo ni maneno machafu yasiyo kuwa na msingi yakuchafuwa kwanza wanamuziki,akalenga ma rapa,akalenga ma Redio na bila kusahau wanahabari.
Track hiyo ambayo mwenyewe Burundiano ameibatiza jina la "My name" yani jina langu kwa lugha ya kiswahili.
Wimbo huwo wa "My name" umetoka baada yakuwa na habari za mvutano kati ya mwanamuziki huyo na mwanamuziki mwenye jina Africa mashariki na rafiki wa karibu na tajiri kutoka Tanzania namzungumzia (Lolilo na Diamond).
Burundiano na Mh Ismail Niyonkuru on Rema Fm |
Wiki moja baadae Mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru aliweza kutobowa kitu ambacho kilikuwa kama kinafichwa na mwanamuziki Burundiano na ikawa kama mkuki wa moto amemchoma mwanamuziki kuhusiana na track ya "My best Friend" ya kwake tena huyo huyo mwanamuziki Burundiano kuwa alitumia beat ya mwwanamuziki kutoka magharibi mwa Africa nchini Nigeria Banky W nakuchanga na style ya track "Am I still that special man" track ya zamani kabisa ya wanamuziki wawili ndugu mapacha kutoka Nigeria nawazungumzia P-Square.
Inasemekana kwa mujibu wa uchunguzi kuwa mwanamuziki huyo Burundiano kitendo hicho alicho kifanya mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru cha kumuumbuwa kwenye redio huku ikiambatanisha kuwa mwanahabari huyu kwa sasa anakuja juu nakusikilizwa zaidi na mamia ya raia wa hapa nchini Burundi.
Siku hiyo mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru aliweza kuruhusu sim 5 ziweze kuchangia kuhusu hizo track 2 ambazo Burundiano ameweza kuwa ame copy na ku paste na majibu ya simu hizo yalijibu kuwa ni ndio mwanamuziki Burundiano ka copy na kupaste.
Kuanzia siku hiyo uhusiano kati ya Mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru na mwanamuziki Burundiano uliweza kuingia dosari huku mwanamuziki huyo aliweza kuongea kwa njia ya sim siku hiyo hiyo na mkurugenzi wa vipindi vya Redio anayo ifanyia kazi mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru kwa siri na mwanamuziki huyu kuhisi kuwa mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru asijuwe lolote kama amemsheta kwa Boss wake nakumwambia Boss wake kuwa hataki tena mtangazaji huyo arudi kucheza nyimbo zake kwenye vipindi vyote anavyo viendesha,ila Kiongozi huyo ambae jina lake linahifadhiwa aliweza kumuhoji kwanini umechukuwa huyo uwamuzi ila mwanamuziki huyo inasemekana alisalia bila kuongea huku akigugumiza kwenye sim.
Muda mchache baadae kwenye siku hiyo hiyo Mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru aliweza kuitwa na kiongozi huyo ofisini mwake ili kuambiwa ujumbe ambao Burundiano ameutuma kupitia boss wake.
Mh Ismail Niyonkuru aliweza kufikishiwa ujumbe huwo ila mtangazaji huyo aliweza kumuuliza swali lakibusara boss wake pale alipo muuliza kuwa Burundiano alimwambia sababu za yeye kuamuwa hivo ila Boss wake alimjibu nakumwambia kuwa na yeye alijaribu kumuuliza Burundiano ila hakuweza kumjibu.Mh Ismail Niyonkuru aliona si vyema kusalia na ukweli moyoni nakuamuwa kumwambia Boss wake sababu haswa za mwanamuziki huyo kuamuwa hivo huku akimsikilizisha nyimbo hizo 3 ikiwemo na hiyo ya Burundiano,Kiongozi huyo aliweza kuchekaa sana huku akisema "kwani hichi ndo anacho kuchukulia mbona hizi nyimbo zinafananaa" alisikika akisema Boss huyo.
Burundiano na Mh Ismail Niyonkuru |
Kitu hicho kimeambatanisha na kile alicho kisema mwanahabari Raphael Nyandwi wa Redio Salama na Televisheni kwenye kipindi cha huyo huyo mtangazaji Mh Ismail Niyonkuru akiwalenga wale wanamuziki wanao ingia studio kwenda ku rekodi nyimbo zakuwachafuwa wenzao huku wakishindwa kuandika mashahiri yakujenga jamii,hayo aliyasema baada yakuwa na fununu kuwa kuna ngoma ambayo inaitwa "Bwana Yahaya" ambayo bado hadi sasa haijatoka yenye ujumbe wakuwalenga tena wengine japo haina maneno ya utovu wa nidhamu kama hii ya "My name"
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!