Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KAMA ULIKUWA HAUFAHAM BASI TAMBUA KUWA AY NDIE ALIE MKUTANISHA RAPA MADEE NA P-UNIT NA KUTENGENEZA BONGE LA TRACK

KAMA ULIKUWA HAUFAHAM BASI TAMBUA KUWA AY NDIE ALIE MKUTANISHA RAPA MADEE NA P-UNIT NA KUTENGENEZA BONGE LA TRACK

Written By Unknown on Sunday, 16 February 2014 | Sunday, February 16, 2014

Msanii wa Tip Top Connection, Madee ameelezea jinsi ambavyo ilifanyika remix ya hit yake iliyoteka chart ya nyimbo bora ya radio nyingi nchini Tanzania mwaka jana ‘Pombe Yangu/Sio Mimi’.
Madee amesema kuwa ilikuwa ni ndoto yake mwaka huu kufanya collabo na msanii wa kimataifa au wa nje ya nchi kwa kuwa alikuwa hajawahi kufanya hivyo tangu aanze muziki, na kwamba wazo lake la kwanza la kufanya remix ya wimbo huu ilikuwa afanye na Prezzo wa Kenya.
“Ambaye amesaidia kwa msaada mkubwa sana alikuwa ni Ambwene Yesaya (AY), mimi nilimwambia nataka kufanya na Prezzo lakini AY akasema Prezzo kwa sasa hivi ratiba yake haiko vizuri kwa sababu ya habari zake na nini, kwa hiyo tufanye na P-Unit. Na mimi aliponitajia P-Unit nikafurahi, lakini nilikuwa sijawahi kukutana na hao jamaa sasa tutafanyaje, akasema wewe usijali niachie mimi.” Amesema Madee.
Amedai kuwa baada ya hapo, AY alimsaidia kumuunganisha na P-Unit ambapo yeye ndiye aliyesimamia zoezi la kutuma beat Nairobi kwa P-Unit na kisha kuirudisha kwa Marco Chali ambaye alimaliza na Madee.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi