Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha tangazo la
kuundwa kwa serikali mpya nchini Lebanon, na kumpa heko Waziri Mkuu
Tamam Salam kwa hatua hiyo muhimu.
Taarifa ilotolewa Jumamosi na Msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa Ban amewahimiza viongozi wa kisiasa wa Lebanon kuendeleza mazungumzo ya kujenga yalochangia kuundwa kwa serikali hiyo mpya, na kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao wa urais unaendeshwa vyema katika msingi ilowekwa kisheria. Ban amempongeza Waziri Mkuu anayeondoka, Najib Mikati kwa uongozi wake.
Jana Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Tammam Salam alitangaza kuunda serikali mpya ya masikilizano baada ya miezi kumi ya mkwamo wa kisiasa. Serikali hiyo ya umoja inajumuisha wanachama wa harakati ya Hizbullah na kambi ya waziri mkuu wa zamani Sa’ad Hariri. Lebanon imekuwa bila serikali tokea mwezi Aprili mwaka jana kutokana na hitilafu baina ya Hizbullah na Chama cha Mustakabli cha Hariri kuhusu kadhia ya Syria. Kambi ya Hariri inawaunga mkono wapinzani wa rais Bashar Assad wa Syria huku Hizbullah ikimuunga mkono rais wa Syria.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!