Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA MZEE BAN KI-MOON ATANGAZA MIKAKATI YA UN YAKUIMARISHA USALAMA NCHINI AFRICA YA KATI

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA MZEE BAN KI-MOON ATANGAZA MIKAKATI YA UN YAKUIMARISHA USALAMA NCHINI AFRICA YA KATI

Written By Unknown on Friday, 21 February 2014 | Friday, February 21, 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelihutubia Baraza la Usalama na kutoa mapendekezo sita ya kuimarisha amani na ulinzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako hali ya usalama inazidi kuzorota kila siku.
Ban amesema pamoja na uwepo wa askari wa Muungano wa Afrika, MISCA na Ufaransa bado changamoto ni kubwa ya usalama kwani hawezi kuwepo maeneo yote na hivyo wananchi ili kuokoa maisha yao wanaokimbia makazi yao na kukumbwa na madhila ya mateso na hata kuuawa.
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuimarishwa kwa vikosi vilivyopo hivi sasa kwa kupatiwa vifaa pamoja na kuongezwa kwa askari na polisi 3000, vikosi vyote vya kimataifa huko CAR viwe na mratibu mmoja ili kuimarisha utendaji, na tatu askari wanaoongezwa wapatiwe vifaa vya kisasa akisema gharama kwa miezi sita ni dola Bilioni 38.
Hali kadhalika ametaka usaidizi wa fedha kwa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kuimarisha taasisi za usalama na mahakama. Ripoti zinasema kuwa magenge ya magaidi Wakristo wenye misimamo mikali wamewaua maelfu ya Waislamu nchini humo huku mamia ya maelfu wakilazimika kukimbilia katika nchi jirani. Kuna askari 1,600 wa  Ufaransa na maelfu ya askari wengine wa kulinda amani kutoka nchi za Kiafrika huko Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini wameshindwa kuzuia mauaji ya Waislamu yanayofanywa na magaidi Wakristo wenye misimamo mikali.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi