Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KUTOKANA NA MAONI YA WADAU KUHUSU VIPENGELE VYA TUZO ZA KILI MUSIC HATIMAYE ZA MWAKA HUU ZAKOSOLEWA

KUTOKANA NA MAONI YA WADAU KUHUSU VIPENGELE VYA TUZO ZA KILI MUSIC HATIMAYE ZA MWAKA HUU ZAKOSOLEWA

Written By Unknown on Monday, 17 February 2014 | Monday, February 17, 2014

Ni time ya kufahamu kuhusu tuzo ambazo hutolewa kwa Wanamuziki/Wasanii mbalimbali wa Tanzania zikiwa zimeanzishwa mwaka 1999 ambapo za mwaka huu 2014 zimezinduliwa leo February 17 2014.
George Kavishe
Mabadiliko yatakayoonekana kwenye msimu huu ni kutokana na maoni na mapendekezo ya wadau wa tasnia ya muziki, kutakua na vipengele 36 ambapo 34 ni za kuchaguliwa na mbili zilizobaki ni zile maalum za kuteuliwa.
Mwaka 2013 kulikua na vipengele 37 ambapo Mwaka huu imeondolewa category moja kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki, ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.
Category zilizobadilishwa majina ni Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki, mwaka jana ilikua msanii bora wa kike, mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.
Mwimbaji bora wa kike band ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kike band ambapo hii ni kutokana na neno ‘msanii’ kuingiliana na usanii wa ujuzi mwingine wa ubunifu.
Kwa sasa kutakua na video bora ya muziki ya mwaka ambayo mwaka jana ilikua video bora ya wimbo, wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongopop, mwaka huu pia kutakua na wimbo bora wenye vionjo vya asili vya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi