Ufaransa
ina mpango wa kuongeza wanajeshi mia nne zaidi ili kuimarisha
oparesheni za kiusalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Rais wa nchi
hiyo, Francois Hollande amesema Paris inaongeza idadi hiyo ili kufikisha
wanajeshi 2000 nchini humo.
Rais Hollande pia ameutaka Umoja wa Ulaya EU kuharakisha mpango
wa upelekaji wa wanajeshi wake 500 huku akiahidi kuwa serikali yake
itaendeleza jitihada za kukomesha mauaji, unyanyasaji na kurejesha
usalama.
Kwa upande wake Mkuu wa sera za nje wa EU, Catherine Ashton amesema wamejipanga kutekeleza ahadi hiyo na kuwa wanajeshi hao watawasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hivi karibuni.
Wanadiplomasia wa Ulaya wanasema majeshi hayo yataanza kuingia mjini Bangui mwezi ujao, baada ya mapema juma hili Mawaziri wa EU kuipa oparesheni hiyo muda wa miezi tisa.
Mbali na Ufaransa, nchi tano wanachama wa EU wamejitolea kushiriki mpango huo, wakati mataifa makubwa kama Uingereza na Ujerumani yakikataa kuahidi iwapo yataoa wanajeshi wake kwenye oparesheni hiyo.
Jitihada hizo zinakuja wakati shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF likisema watoto 133 wameuawa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, baadhi yao wamechinjwa na wengine wamebaki na ulemavu.
Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa katika machafuko toka Muungano wa waasi wa Seleka ulipomuondoa madarakani Rais Francois Bozize mwezi Machi mwaka jana na kumuweka madarakani kiongozi wao wa kiislamu Michel Djotodia aliyejiuzulu kwa shinikizo mwezi uliopita.
Rais mpya wa mpito Catherine Samba Panza ameahidi kukabiliana na makundi ya wapiganaji likiwemo la Kikristo la anti-balaka ambalo limekuwa likituhumiwa kwa uvunjifu wa amani.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!