Usiku
wa jumatano ulikuwa mrefu sana kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya
timu yao kupigiwa soka la hatari na kufungwa 2-0 na mabingwa watetezi wa
klabu bingwa ya ulaya FC Bayern Munchen.
Usiku huo tulishuhudia Bayern Munich wakiweka rekodi mpya ya Champions
League baada ya kukamilisha asilimia 95% ya pasi walizopiga.
Tuangalie ushindi huo wa Bayern kupitia mfumo wa namba.
863
Hii
ni namba ya pasi walizojaribu kupiga Bayern, 95% ya pasi hizi zilifika
kwa wenzao. Hii ni rekodi mpya katika champions league tangu utaratibu
wa takwimu kwenye mechi uanze msimu wa 2003-04 season..
222
Namba
ya pasi walizojaribu kupiga Arsenal. Walikamilisha 71% ya pasi hizo.
Namba ya chini kabisa kwa Arsenal katika takwimu za pasi, kabla ya jana
namba ya chini kabisa ilikuwa 394, hii ilikuwa kwenye EPL dhidi ya
Tottenham mwezi September mwaka jana.
147
Hii namba ya pasi alizopiga kiungo wa Bayern Toni Kroos.
127
Namba ya pasi alizopiga Toni Kroos katika nusu ya uwanja golini mwa Arsenal - alikamilisha 96.1% ya pasi hizo.
100
Goli
la Toni Kroos jana usiku lilikuwa goli la 100 kwa Bayern Munich katika
mashindano yote msimu huu. Kadi nyekundu ya golikipa Wojciech Szczesny
ilimfanya kuwa mchezaji wa 100 kupewa kadi nyekundu tangu Wenger aanze
kuifundisha timu hiyo mwaka 1995.
78.8
Asilimia ya umiliki wa mpira waliyokuwa nayo Bayern Munich ndani ya dakika 90.
30
Mchezaji
aliyejaribu kupiga pasi nyingi zaidi kwa upande wa Arsenal alikuwa Jack
Wilshare ambaye alikamilisha 66% ya majaribio 30.
26
Majaribio
ya kufunga yaliyofanywa na Bayern katika goli la Arsenal, Arsenal
walijaribu mara 8 tu - mara 1 tu katika kipindi cha kwanza.
12
Arsenal waliweza kuwa na jumla ya 12% ya kumiliki mpira katika kipindi cha pili.
3
Winga
wa Bayern Munich Arjen Robben ndio mchezaji pekee kuwahi kupewa penati 3
katika msimu huu wa Champions league. Mesut Ozil ndio mchezaji pekee
aliyekosa mara mbili.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!