Nchi tatu za Afrika Mashariki zimezindua 'Viza ya Pamoja ya Utalii'
ambapo kuanzia sasa watalii wanaotembelea Uganda, Kenya na Rwanda
watahitaji viza moja tu badala ya viza ya kila nchi wakati
wakizitembelea nchi hizo tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hiyo ni
kufuatia kuzinduliwa Visa ya Pamoja ya Utalii Afrika Mashariki katika
hafla iliyofanyika Kampala hiyo jana na kuhudhuriwa na marais Yoweri
Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Museveni amesema viza hiyo itaimarisha zaidi ushirikiano wa kisiasa baina ya nchi wanachama na Rais Kenyatta amesema viza hiyo ni mwanzo wa usafiri huru wa watu na bidhaa. Rais Kagame naye amesema kuzinduliwa viza hiyo ni ishara ya azma ya kuimarisha ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Viza hiyo inayotumika kwa siku 90, itagharimu dola za kimarekani 100, na watalii wanaweza kuomba viza hiyo katika ofisa yoyote ya uhamiaji ya Uganda, Kenya na Rwanda au kwenye mtandao wa internet. Burundi na Tanzania bado hazijajiunga na mpango huo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!