Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SERIKALI YA BWANA GOODLUCK HAINA NGUVU MBELE YA KUNDI LA BOKO HARAM:KASHIM SHETTIMA

SERIKALI YA BWANA GOODLUCK HAINA NGUVU MBELE YA KUNDI LA BOKO HARAM:KASHIM SHETTIMA

Written By Unknown on Tuesday, 18 February 2014 | Tuesday, February 18, 2014

Gavana wa jimbo la Borno nchini Nigeria amesema kuwa, kundi la Boko Haram lina nguvu kuliko jeshi la nchi hiyo. Kashim Shettima amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo na kusisitiza kwamba, wanamgambo wa Boko Haram wana nguvu na wamejizatiti zaidi kuliko hata jeshi la nchi hiyo.
Ameongeza kuwa, ni vigumu kwa jeshi la Nigeria kuweza kuwashinda na kuwasambaratisha wanamgambo wa Boko Haram. Hivi karibuni kundi la Boko Haram lilifanya mashambulio makubwa katika jimbo la Borno na kuwauwa kwa akali watu 100.
Harakati za kundi la Boko Haram zimekuwa zikiinyima usingizi serikali ya Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ambaye sasa anakabiliwa na mashinikizo ya kila upande kutokana na serikali yake kushindwa kulitokomeza kundi hilo.
Wakosoaji wa serikali ya Nigeria wanamlaumu Rais wa nchi hiyo wakisema kwamba, ameshindwa kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram licha ya kutangaza hali ya hatari katika majimbo kadhaa likiwemo la Borno kwa lengo la kuendesha operesheni za kijeshi dhidi ya kundi hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi