Maelfu ya polisi wanaendelea kupambana na waandamanaji
wanaoipinga serikali ya Thailand katika mji mkuu Bangkok. Afisa mmoja wa
polisi ameuawa katika vurugu hizo huku watu 42 wakijeruhiwa baada ya
vyombo vya usalama kuvamia maandamanao ya wapinzani. Waandamanaji hao
wanaonekana wakiwa wamejikusanya katika maeneo muhimu ya mji mkuu
Bangkok.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, polisi wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika karibu na jengo la serikali mjini Bangkok.
Meja Jenerali Adul Saengsingkaew amesisitiza kuwa ni lazima waandamanaji hao waruhusu uchukuzi na hali ya kawaida kurejea katika mji mkuu. Waandamanaji wasiopungua 100 wametiwa mbaroni na vyombo vya usalama tangu mwezi Desemba mwaka jana. Waandamanaji hao wanapinga serikali ya Waziri mkuu Yingluck Shinawatra.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!