Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » TAARIFA KUTOKA SAUDI ARABIA ZASEMA KUWA BEI YA BIDHAA IMEPANDA HALI AMBAYO IMEANZA KUWATIA HOFU WANANCHI WAKE

TAARIFA KUTOKA SAUDI ARABIA ZASEMA KUWA BEI YA BIDHAA IMEPANDA HALI AMBAYO IMEANZA KUWATIA HOFU WANANCHI WAKE

Written By Unknown on Tuesday, 18 February 2014 | Tuesday, February 18, 2014

Kuongezeka kwa kasi bei ya bidhaa mbalimbali nchini Saudi Arabia, kumewatia wasi wasi mkubwa wananchi wa nchi hiyo. Ongezeko hilo ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini humo limewafanya wananchi wengi kuingiwa na wasi wasi na kuilalamikia hali hiyo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, vyakula na bidhaa nyingine muhimu zimepanda bei katika miezi ya hivi karibuni. Ongezeko la bei za bidhaa linafikia asilimia 30 na kwamba, mwenendo wa kupanda kwa bidhaa hizo ungali unaendelea.
Kutokana na kuongezeka bei za bidhaa muhimu, ongezeko la bei nchini Saudia mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana linakadiriwa kufikia asilimia tatu. Shirika la Takwimu la Saudi Arabia limetangaza katika ripoti yake ya kila mwezi kwamba, ongezeko la vifaa vya nyumbani ni sawa na asilimia sita, vyakula asilimia 5, nyuma, maji, umeme, gesi na nishati nyingine asilimia 3.7 huku huduma za nyumba za kulala wageni na hoteli likifikia asilimia 2.7.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, umasikini na ukosefu wa ajira unazidi kupanuka nchini Saudia huku maelfu ya watoto wa familia ya Kifalme wamekuwa wakipora utajiri wa kitaifa wa nchi hiyo kwa ajili ya kujiandalia maisha ya anasa na starehe ndani na nje ya nchi hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi