Mtu mmoja aliyejitambulishwa kwa jina la Shariff, amekiambia kipindi
cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm kuwa yeye ni mganga anayemrekebishia
mambo AT, na kwamba msanii huyo alimpangishia nyumba maeneo ya Kijiwe
Samli, Dar es Salaam baada ya kuona kwamba anamfanyia mambo na
anafanikiwa kimuziki. Lakini baada ya muda msanii huyo aliacha kulipia
kodi ya nyumba ambayo imefikia kiasi cha shilingi laki tisa na kwamba
kwa sasa amemtelekeza.
Hata hivyo, msanii huyo alipoulizwa na Edson Mkisi wa Times FM kuhusu tuhuma hizo na maelezo ya mtu huyo, alimkana na kudai kwamba mtu huyo anatafuta ‘kick’ na kwamba hamfahamu kabisa. Lakini aliongeza kuwa kama kweli ni mganga wake aliyempandisha basi amshushe.
“Mimi huyo mtu simjui kabisa sina mjomba kama huyo kama unabisha nikupe namba ya mama yangu umuulize kama mimi ninamjomba wa namna hiyo,huyo jamaa atakuwa anatafuta kick tu ya kuenesha maisha yake hapa mjini lakini mimi simjui hata kidogo.” Alieleza AT.
Mganga huyo aliporudishiwa majibu ya AT na kutakiwa kuthibitisha kile anachokizungumza kwa kutoa ushahidi alisisitiza kufahamiana na AT na kwamba hakutaka watu wajue, “mpaka watoto wadogo kwenye nyumba nayokaa mimi wanamjua…yeye kaongea kwa alivyo kuifurahisha nafsi yake lakini, yeye kila mtu anamfahamu kwamba anakuja kwangu, na mpaka siku ya mwisho amekuja amevaa baibui…baibui la kike ili watu wasimuone.”
Alipoelezwa kuhusu suala lililoelezwa na AT kuwa kama yeye ni mganga aliyempandisha basi amshushe, mtu huyo alisema kuwa taaluma yake hairuhusiwi kumtisha mtu lakini kama ameweza kumsikia amefika kwenye media labda anaweza kumuelewa na wakaongea kistaarab ili wajue wanafanya vipi kulimaliza deni hilo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!