Siku kama ya leo miaka 541
iliyopita alizaliwa mnajimu na mwanahesabati mashuhuri wa Poland
Nicolaus Copernicus. Awali alijifunza elimu ya nujumu na baadaye tiba,
na baada ya kukamilisha masomo alianza kufundisha hesabati huko Roma.
Hata hivyo Copernicus aliendelea kudurusu na kufanya utafiti wa elimu ya
nujumu na mwaka 1503 alivumbua nadharia ya harakati ya dunia kuzunguka
jua na pia dunia kujizunguka yenyewe katika kila baada ya masaa 24.
Nicolaus Copernicus alifariki dunia tarehe 24 Mei 1543 siku chache tu
baada ya kuchapisha kitabu cha On the Revolutions of the Celestial
Spheres kinachofafanua nadharia zake.
-------------------------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 17 iliyopita alifariki dunia Deng Xiaoping, kiongozi wa zamani wa China na mhandisi wa mageuzi ya kiuchumi na kisiasa ya nchi hiyo. Katika kipindi cha uongozi wa Xiaoping China ilifanya mageuzi makubwa katika nyanja mbalimbali na alifanya marekebisho makubwa katika uchumi wa kisoshalisti wa wakati huo wa China na kuuelekeza kwenye uchumi wa soko. Wakati huo China ilifanikiwa kuingia katika nyanja mbalimbali za kimataifa na kutatua migogoro iliyokuwepo katika uhusiano wake na nchi kadhaa. Deng Xiaoping alijiuzulu mwaka 1990 kutokana na maradhi na umri wake mkubwa na hadi anafariki dunia alikuwa akihesabiwa kuwa shakhsia mkubwa zaidi wa China.
--------------------------------------------------------------------------------------------
Na miaka 4 iliopita katika
siku kama ya leo yaani tarehe 30 Bahman 1388 Hijiria Shamsia, manoari ya
kwanza ya kivita ya Iran inayojulikana kwa jina la Jamaran ilianza
kufanya kazi. Jamaran ni manoari ya kijeshi yenye uwezo wa kubeba aina
kadhaa za makombora ya kuhujumu meli na kutungua makombora na ndege za
adui. Pia ina rada za kisasa na uwezo wa kushiriki katika vita vya
kielektroniki. Meli hiyo inayoenda kwa kasi kubwa pia ina eneo la kutua
helikopta.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!