Thabo Mbeki, mkuu wa kamati ya upatanishi ya Umoja wa Afrika
katika mgogoro wa Sudan ametangaza kuwa umoja huo umeipa serikali na
waasi wa nchi hiyo muda wa siku 10. Sambamba na kuashiria kusimamia
mazungumzo kati ya serikali ya Khartoum na waasi yaliyokuwa yakifanyika
kwa lengo la kuhitimisha vita katika eneo la Kordofan na Blue Nile,
Umoja wa Afrika umezipa pande mbili hizo hasimu muda wa hadi siku 10 ili
kuanza tena mazungumzo hayo. Akielezea sababu za kusimama mazungumzo
hayo, Mbeki amesema kuwa mazungumzo hayo yamesimama kutokana na Harakati
ya Ukombozi wa Watu wa Sudan, tawi la kaskazini (SPLM-N) kusisitiza
kufikiwa makubaliano kuhusu masuala yote, huku upande wa serikali
ukisisitiza kufikiwa tu makubaliano juu ya maeneo ya Kordofan na Blue
Nile.
Tangu mwaka 2011 maeneo ya Kordofan kusini na Blue Nile ya kusini mwa Sudan yamekuwa yakishuhudia mapigano kati ya waasi wa harakati ya SPLM kaskazini na serikali ya Khartoum.
Tangu mwaka 2011 maeneo ya Kordofan kusini na Blue Nile ya kusini mwa Sudan yamekuwa yakishuhudia mapigano kati ya waasi wa harakati ya SPLM kaskazini na serikali ya Khartoum.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!