Siku kama ya leo miaka 133
iliyopita alifariki dunia mwanahistoria, mwanafalsafa na mtaalamu
mashuhuri wa masuala ya mashariki wa Scotland Thomas Carlyle.
Mwanafalsafa huyo alizaliwa mwaka 1795 na mbali na lugha ya Kijerumani,
alijifunza pia lugha ya Kiarabu. Katika safari zake nyingi katika nchi
za Kiislamu, mwanahistoria huyo alijifunza utamaduni na ustaarabu wa
Kiislamu na kuathirika mno na dini hiyo. Thomas Carlyle anasema kuhusu
Qur'ani kwamba: "Qur'ani ni sauti isiyokuwa na wasita kutoka kwenye roho
ya ulimwengu, na wanadamu wanapaswa kuisikiliza, la sivyo hawapaswi
kusikiliza maneno mengineyo."
Na miaka 168 iliyopita katika
siku kama ya leo mwafaka na tarahe 5 Rabiul Thani mwaka 1267 Hijiria,
gazeti la kwanza la lugha ya Kifarsi lililoitwa 'Waqai'e Itifaqiyeh'
lilianza kuchapishwa mjini Tehran. Gazeti hilo lilianza kuchapishwa
wakati wa kutimia mwaka wa tatu wa ufalme wa Nasiruddin Shah Kajjar, kwa
amri ya Kansela Mirza Taqi Khan Amir Kabiri. Gazeti hilo lilikuwa
likiandika habari za utawala wa wakati huo wa Iran, dunia na makala za
kisayansi zilizokuwa zikitafsiriwa kutoka kwenye magazeti ya Ulaya.
Gazeti la 'Waqai'e Itifaqiyeh' lilichapishwa hadi toleo nambari 472 na
baada ya hapo likaendelea kuchapishwa kwa majina tofauti.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!