Rais Moncef Marzouki wa
Tunisia amesifu kupasishwa katiba mpya nchi nchi hiyo na kuitaja hatua
hiyo kuwa ni ushindi wa tatu kwa taifa hilo. Akizungumza hii leo katika
sherehe za kupasishwa rasmi katiba hiyo zilizohudhuriwa pia na viongozi
wa nchi mbalimbali duniani, al Marzouki amesema, ushindi wa kwanza wa
wananchi wa Tunisia ni kumpindua dikteta kulikofanywa na vijana
waliojitolea mhanga nafsi zao na ushindi wa pili ni mapambano dhidi ya
magaidi waliokuwa wakitaka kuleta machafuko nchini humo. Katiba mpya ya
Tunisia yenye vifungu 149 ilipasishwa siku kadhaa zilizopita na Bunge
la katiba la nchi hiyo. Katiba hiyo imetajwa kuwa ni mfano mzuri kwa
nchi nyingine za Kiarabu ambazo pia zimeshuhudia harakati za Mwamko wa
Kiislamu.
Miongoni mwa vifungu vya kuvutia katika
katiba hiyo mpya ni kuitaja Tunisia kuwa nchi ya Kiislamu, lugha yake
rasmi kuwa ni Kiarabu na kwamba rais wa nchi hiyo pia anapaswa kuwa
Muislamu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!