Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetahadharisha kuwa
jamii ya Waislamu katika miji mingi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati
wanakabiliwa na hatari ya kulengwa na mashambulio ya ulipizaji kisasi.
Shirika hilo limesema kuwa, machafuko nchini humo yamefikia kiasi
ambacho hakijawahi kushuhudiwa na kwamba maelfu ya Waislamu tayari
wamekimbilia katika nchi za Chad na Cameroon. MSF limeongeza kuwa,
jamii zote zimeathiriwa na machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
lakini hivi sasa Waislamu ndio wanaoshambuliwa kwa wingi na kwamba wana
wasiwasi na mustakbali wa watu wanaoishi kwenye vijiji vilivyozungukwa
na makundi ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka.
Ripoti zinasema kuwa, katika mji mkuu Bangui mapigano na uporaji unaendelea huku maelfu ya Waislamu wakiukimbia mji huo hii leo na kusindikizwa na askari wa kulinda amani wa Chad. Wanamgambo wa Kikristo wanadaiwa kuendeleza mashambulizi dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa msaada wa askari wa Ufaransa walioko nchini humo, huku Waislamu wakibaki bila ulinzi baada ya kufurushwa waasi wa Seleka.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!