Miaka 35 iliyopita katika siku kama ya leo wananchi Waislamu wa Iran
kama ilivyokuwa katika siku za kabla yake, walikusanyika kwa wingi na
kuelekea katika makazi ya Imam Khomeini mjini Tehran ambapo walionana
naye na kutangaza utiifu wao kwake. Siku hiyo wananchi wa Iran
walishikamana na kuwa kitu kimoja na hamasa yao ilibashiri tukio muhimu nchini nchini humo. Mbali na matabaka mbalimbali ya wananchi waliokwenda
kuonana na Imam, vikosi mbalimbali vya jeshi pia vilikwenda kumuona
kiongozi wa harakati za mapinduzi na kumtambua Imam kuwa Amiri Jeshi
Mkuu. Imam Khomeini alihutubia wananchi wa Iran na kusisitiza juu ya
kufikishwa Shah mahakamani.
Tarehe 7 Februari mwaka 1961 kiongozi wa chama cha Abako, Joseph
Kasavubu aliteuliwa kuwa Rais wa konfederesheni iliyokuwa ikiungwa mkono
na Umoja wa Mataifa ya Congo. Baada ya Congo kupata uhuru kutoka kwa
mkoloni Mbelgiji, Kasavubu alichaguliwa kuwa mkuu wa Baraza la Taifa
lililoanza kazi Juni 30 mwaka 1960. Nchi huru ya Congo ilikumbwa na
misukosuko mingi ya kisiasa baada tu ya kupata uhuru na serikali kuu
ilidumazwa na mivutano iliyotokea kati ya viongozi wake.
*****
Joseph Kasavubu |
*****
Miaka 801 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa, alimu na
mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu wa Iran Qutbuddin Mahmoud bin Dhiyauddin
Masoud Kazeruni, maarufu kwa jina la Mulla Qutb katika mji wa Kazerun nchini Iran. Katika maisha yake msomi huyo alisafiri maeneo mengi ya
dunia. Msomi huyo wa Kiislamu aliandika vitabu vingi vya thamani kama
"Nihayatul Idrak", "Sharh Qanun Ibn Sinaa" na "Sharh Hikmatil Ishraq."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!