KLABU ya Manchester City
imepanga kuongeza Uwanja wake wa Etihad kwa zaidi ya viti 14,000 ambapo
mara baada ya mpango huo kukamilika uwanja huo utakuwa na uwezo wa
kuingiza mashabiki 62,170 badala ya 47,620 kama ilivyo sasa. Mpango huo
tayari umeshawasilishwa katika tume ya mipango ya halmashauri na
kutokana na ripoti iliyotolewa jana mpango huo umekubaliwa. Kama
matengenezo ya uwanja huo yakiendelea jiji la Manchester litakuwa na
viwanja viwili vikubwa nchini Uingereza mwingine ukiwa ni Old
Traford. Man City wamefikia mpango huo ili kuongeza mapato katika
viingilio hususani katika kipindi hiki ambacho timu hiyo inafanya vyema
katika michuano mbalimbali ya ndani na kimataifa.
Home »
michezo ulaya
» TIMU YA MAN-CITY IMO MBIONI KUUPANUWA UWANJA WAO MKUBWA WA ETIHAD AMA UWANJA WA MACHUNIO
TIMU YA MAN-CITY IMO MBIONI KUUPANUWA UWANJA WAO MKUBWA WA ETIHAD AMA UWANJA WA MACHUNIO
Written By Unknown on Friday, 7 February 2014 | Friday, February 07, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!