Sudan Kusini imekadhibisha tuhuma zilizotolewa na wataalamu wa
Umoja wa Mataifa kwamba jeshi la nchi hiyo lilitumia mabomu ya vishada
kwenye vita dhidi ya waasi.
Hivi karibuni timu ya wataalamu wa mabomu ya Umoja wa Mataifa
iliyotembelea nchini humo ilitoa taarifa kwamba yameonekana mabaki ya
mabomu ya vishada pambizoni mwa barabara kuu ya Juba kuelekea mji wa
Bor, makao ya jimbo la Jonglei kaskazini mwa nchi hiyo. Taarifa ya
watalamu wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, mabomu hayo ambayo hurushwa
kwa kutumia ndege za kivita na mizinga huweza kusambaa sehemu kubwa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, mabomu hayo licha ya kuuawa hukatakata vingo
mbalimbali vya mwanadamu.
Wakati huohuo, msemaji wa jeshi la Sudan Kusini amesema kuwa, wanajeshi walio wengi hawana uelewa na taarifa zozote kuhusiana na mada hizo za milipuko. Msemaji huyo ameongeza kuwa jeshi la nchi hiyo halina uwezo wa kutumia silaha kama hizo.
Imeelezwa kuwa kwa akali watu elfu kumi wameuawa kwenye mapigano yaliyotokea Sudan Kusini na mamia ya maelfu ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!