Baraza la mawaziri la Kenya siku ya Alhamisi (tarehe 13 Februari)
liliidhinisha kuanzishwa kwa eneo la biashara huru huko Mombasa ili
kurahisisha biashara ya kanda na kimataifa na kukuza uwekezaji, gazeti
la Daily Nation la Kenya liliripoti.
"Eneo la biashara huru pia kutafungua soko tayari kwa bara pana la Afrika na hivyo kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya nchi," baraza la mawaziri lilisema katika taarifa.
Eneo la biashara huru linatarajiwa kuimarisha biashara ndani ya Afrika kwa kuruhusu bidhaa kuingia katika eneo lisilotozwa ushuru kwa mara ya kwanza, kuongeza kiasi cha biashara ya Kenya na kujenga fursa za ajira kwa vijana.
Pia siku ya Alhamisi, Kenya ilisafirisha nje shehena yake ya kwanza ya tani 25,000 za madini ya iIlmenite, sehemu kubwa ya madini ya titanium, zilizopangwa kuenda China, Capital FM ya Kenya iliripoti.
Waziri wa Madini Najib Balala alisema Wizara ya Madini ilitoa kibali kwa kampuni ya Australia Base Titanium na kuiruhusu kusafirisha nje zaidi ya tani 450,000 za madini ya Ilmenite, zircon na rutile titanium kwa mwaka.
Makubaliano ya usafirishaji nje unatarajiwa kuchangia shilingi bilioni 17.1 (dola milioni 197.8) kwa mwaka katika uchumi wa Kenya.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!