Serikali ya Somalia siku ya Ijumaa (tarehe 14 Februari) iliwachilia wakurugenzi wawili wa redio za binafsi waliokuwa wamekamatwa na Shirika la Usalama wa Taifa baada ya kutangaza na kuchapisha picha za afisa wa serikali aliyejeruhiwa, iliripoti Redio Dalsan ya Somalia.
Mohamed Barre Haji, mmiliki na mkurugenzi wa Redio Dalsan, na Ibrahim Mohamed Yare, mkurugenzi wa Redio Haatuf, walikamatwa usiku wa Jumanne, hatua iliyozusha lawama kutoka Chama cha Waandishi wa Habari cha Somalia na Jumuiya ya Vyombo vya Habari vya Somalia (SIMHA)
"Walikabiliwa na mateso makubwa kutoka kwa shirika la kijasusi, simu zao zilichukuliwa na walitishiwa kunyamazishwa milele ikiwa wataendelea kuandika juu ya serikali," alisema Mwenyekiti wa SIMHA, Hassan Ali Gessey.
Gessey alisema waandishi hao wa habari walikuwa kwenye "eneo la siri mjini Mogadishu kwa usalama wao wenyewe baada ya maafisa wa usalama wa taifa kuvamia vituo vyao."
Aliitolea wito jumuiya ya kimataifa ya haki za binaadamu "kuwaokoa" waandishi hao wawili wa habari ambao wanaripotiwa kujeruhiwa vibaya. Serikali ya Somalia bado haijasema chochote juu ya madai hayo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!