Muigizaji wa filamu za Hollywood ambaye pia ni mshindi wa
tuzo za Oscar, Philip Seymour Hoffman amefariki dunia akiwa na umri wa
miaka 46. Kwa mujibu wa taarifa za polisi, mwili wa Seymour ulikutwa na
rafiki yake, David Katz, ukiwa bafuni nyumbani kwake.
Ripoti hizo zinadai kuwa mwili wake ulikutwa na sindano kwenye mkono wake ikiwa na dawa za kulevya na pia pakiti za madawa hayo zilikuwa karibu naye, hivyo kifo chake kimehusishwa moja kwa moja na matumizi ya madawa ya kulevya kupita kiasi.
Hoffman alishinda tuzo za Oscar mwaka 2006, kupitia filamu ya mwaka 2005 ‘Capote’.
Aliwahi kushiriki katika filamu nyingi zikiwemo, Scent of a Woman, Boogie Nights, The Big Lebowski, Patch Adams, Magnolia, The Talentend Mr. Ripley, Cold Mountain, Before the Devil Knows You’re Dead, The Savages na alionekana kwenye Mission Impossible III.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!