Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » UHUSIANO WA NCHI MBILI BABE DUNIANI AMBAZO NI UFARANSA NA MAREKANI WAONEKANA KUNOGA ZAIDI

UHUSIANO WA NCHI MBILI BABE DUNIANI AMBAZO NI UFARANSA NA MAREKANI WAONEKANA KUNOGA ZAIDI

Written By Unknown on Wednesday, 12 February 2014 | Wednesday, February 12, 2014

Rais wa Marekani Barack Obama amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Ufaransa katika kusimamia upatikanaji wa amani na usalama wa dunia ikiwa ni pamoja na kupambana na vitendo vya kigaidi .Rais Obama amesema Ufaransa chini ya utawala wa Rais Francois Hollande imeonyesha ujasiri katika hatua za kushughulikia migogoro inayozikumba nchi mbalimbali duniani.

Katika mkutano wa pamoja wa na vyombo vya habari, ma rais hao wamepongezana kuhusu kudumisha mahusiano ya kihistoria wapofikia katika ushirikiano licha ya kuwepo kwa mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakiwatofautisha.
Obama ameeleza kuwa ufaransa imejitoa kwa dhati kwenye migogoro ya nchi za Syria, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati na changamoto inayotokana na mpango wa nyuklia wa nchi ya Iran amabayo imekuwa katika mvutano mkali na mataifa yenye nguvu duniani.
Katika hatua nyingine rais huyo wa marekani amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na ushirikiano mzuri na nchi za ulaya bila kubagua kwa kuwa nchi zote ni muhimu.
Kwa upande wake rais Francois Hollande amesema kuwa Ufaransa itaendelea kutoa ushirikiano kwa Marekani ili kushughulikia masuala yanayohusu amani, usalama na vita dhidi ya vitendo vya kigaidi.
katika hatuwa nyingine Rais wa Marekani Barack Obama ametowa tahadhari kwa makampuni ya Ufaransa yanayo kwenda Iran kufanya biashara na taifa hilo wakati huu muafaka juu ya mpango wa Nyuklia wa Iran haujapatikana. Kauli hii ya Obama inakuja wakati huu makampuni ya Ufaransa yamekuwa yakielekea Iran kwa ajili ya mpango wa kuanzisha biashara na taifa hilo.
Mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana, serikali ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani ikiwa ni pamoja na China, Marekani, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Ujerumani walifikia muafaka wa miezi sita huku Iran ikikubali kupunguza urutubishwaji wa Nyuklia, na hivo kupunguziwa pia vikwazo vya kiuchumi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi