Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BADO HADI SASA MISAADA KUWAFIKIA WALENGWA NCHINI SUDAN KUSINI NI MATATIZO KUTOKANA NA WAASI

BADO HADI SASA MISAADA KUWAFIKIA WALENGWA NCHINI SUDAN KUSINI NI MATATIZO KUTOKANA NA WAASI

Written By Unknown on Saturday, 22 March 2014 | Saturday, March 22, 2014

Pande mbili zinazopigana nchini Sudan Kusini zimezuia misaada ya kibinadamu kuwafikia maelfu ya raia ambao waliyakimbia makazi yao tangu miezi mitatu iliyopita kufuatia mzozo huo,afisa moja wa Umoja wa mataifa amearifu.

Takribani magari 50 yaliyobeba misaada mbalimbali ikiwemo vyakula na madawa yamekwama kuingia katika taifa hilo lenye makabiliano huku waasi na serikali wakichelewesha misaada hiyo kuingia.
Hali imekuwa ngumu kwa wafanyakazi wa misaada waliopo katika maeneo ya mapigano huko sudan ambapo jana Mfanyakazi mmoja wa shirika la kimataifa la msalaba mwenkundi la CICR ameuwa jijini Darfour wakati huu vurugu zikiendelea kuripotiwa huko magharibi mwa Sudani.
Najmaddin Salih Musa Bishara, ambaye alikuwa anafanya kazi katika ghala la shirika hilo la msalaba mwekundu aliuawa kwa kupigwa risasi.
Katika taarifa iliotolewa na shirika hilo haikuweka wazi kuhusu hatma ya wafanyakazi wengine waliokuwemo katika gari la shirika hilo. Tangu Februari Mosi mwaka huu serikali ya Kharthoum ilisitisha shughuli za shirika hilo la kimataifa la msalaba mwekundu CICR ikilituhumu kuvuka mpaka katika kutekeleza shughuli zake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi