Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » BAADA YA RAPA LORD EYEZ KUTOKA NCHINI TANZANIA KUWEKWA MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA LAPTOP BASI HIKI NDICHO ALICHO KISEMA MSEMAJI WA KUNDI LA WEUSI

BAADA YA RAPA LORD EYEZ KUTOKA NCHINI TANZANIA KUWEKWA MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA LAPTOP BASI HIKI NDICHO ALICHO KISEMA MSEMAJI WA KUNDI LA WEUSI

Written By Unknown on Wednesday, 5 March 2014 | Wednesday, March 05, 2014

Msemaji wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema kuwa rapper Lord Eyez amesimishwa kazi katika kampuni hiyo na kwamba kwa sasa sio ‘member’.

 “Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi kikampuni.” Amesema Nikki wa Pili na kusisitiza kuwa hajafukuzwa kazi bali amesimamishwa.
Hata hivyo, Nikki wa Pili hakuwa tayari kuweka wazi moja kwa moja sababu zilizopelekea Weusi kumsimamisha kazi rapper huyo.

“Hizo ni confidential, ni issue za kampuni hatuwezi kuziweka wazi lakini Lord Eyez tumemsimamisha kazi hiyo ndio taarifa ambayo tunaitoa kwa media.” Nikki wa Pili ameeleza.
Ameongeza kuwa kwa sasa matukio yote yanayotokea kwa upande wa Lord Eyez yatakuwa yanamhusu yeye binafsi na hayatakuwa na uhusiano wowote na kampuni.
Hii inamaanisha hivi sasa Weusi inaundwa na Joh Makini, Nikki wa Pili, G-Nako na Bonta.

Uamuzi huo wa Weusi umekuja wakati ambapo kumekuwa na taarifa kuwa Lord Eyez alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi Jumamosi, huko Arusha na baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa anatuhumiwa kwa wizi wa laptop aina ya 'Dell'.
Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza kumsamehe msanii huyo.
Weusi walichukua dhamana ya kumtetea na kumuwekea mwanasheria huku wakifanya mikutano na waandishi wa habari ili kuitengeneza image ya kampuni hiyo ambayo ilikuwa imewekewa alama na tuhuma za Lord Eyez ambaye ni member wa kundi la Nako 2 Nako.  

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi