Nyoka huyo alijipindua kwa Mamba na kumbana hadi akafa Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpindua na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra,
karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya
Jumapili.
|
Chatu huyo alianza kumla Mamba na kuwashangaza wakazi wa eneo hilo!!! |
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipindua kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
|
Nyoka huyo alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji |
Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake Tiffany
Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha
hizi."lilikuwa jambo la ajabu sana,'' aliambia BBC "tulimuona Nyoka
akipambana na Mamba , alifanikiwa
kumpindua mamba na kumzungusha hasa katika sehemu ya miguu yake ili
kumdhibiti.''
"pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa
anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka
alikuwa amembana sana.'' "baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kunza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua Nyoka dakika kumi na tano kumla yule Mamba.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na
hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye
hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce
Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu masaa
5. Hatimaye wote walionekana kuchoka.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!