Siku kama ya leo miaka 187 iliyopita,
sawa na tarehe 5 Machi 1827 alifariki dunia Alessandro Volta, mtaalamu
wa fizikia wa Italia akiwa na umri wa miaka 83. Sambamba na kufundisha
katika chuo kikuu, Volta alikuwa akifanya uhakiki na alifanikiwa
kutengeneza chombo cha kupimia kiwango cha umeme Electrometre.
Miaka 61 iliyopita katika siku kama ya
leo mwafaka na tarehe 5 Machi mwaka 1953, alifariki dunia Joseph Stalin,
kiongozi na dikteta wa Urusi ya zamani. Stalin alizaliwa mwaka 1879
nchini Georgia na alijiunga na mrengo wa kikomunisti baada ya kusoma
fikra za mrengo huo. Joseph Stalin alipelekwa uhamishoni huko Siberia
mwaka 1913 kutokana na harakati zake za kisiasa dhidi ya serikali ya
wakati huo ya Urusi. Stalin alibakia huko hadi baada ya ushindi wa
Mapinduzi ya Urusi mwaka 1917. Alipata vyeo vya ngazi za juu wakati wa
uongozi wa Lenin na alishika uongozi wa nchi hiyo akiwa pamoja na
wanasiasa wengine mashuhuri baada ya kufariki dunia Lenin. Mwaka 1927
Stalin aliwafutilia mbali wapinzani wake ndani ya chama na kuwa kiongozi
asiye na mpinzani katika Chama cha Kikomunisti. Joseph Stalin
aliendelea kuwafuta na kuwaangamiza bila ya huruma wapinzani wake ndani
na nje ya chama hicho.
Na siku kama ya leo miaka 46 iliyopita
sawa na tarehe 14 Esfand mwaka 1346 kwa mujibu wa Kalenda ya Kiirani,
alifariki dunia dakta Muhammad Musaddiq, Waziri Mkuu na mmoja wa
wanasiasa mashuhuri wa Iran. Alizaliwa mjini Tehran mwaka 1261 Hijria
Shamsia. Mwaka 1299 Hijria Shamsia ikiwa ni baada ya kuhudumu kama
Waziri wa Fedha na Waziri wa Mambo ya Nje, Musaddiq alichaguliwa kuwa
mwakilishi wa watu wa Tehran bungeni. Hata hivyo baada ya muda mfupi
alijiondoa kwenye uwanja wa siasa na kurejea baadaye mwaka 1322.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!