Umoja wa Afrika umesisitiza ulazima wa kukomeshwa mauaji ya raia
wasio na hatia katika baadhi ya nchi za bara la Afrika. Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma amesema,
taasisi hiyo inatiwa wasiwasi na vitendo vya kigaidi na kikatili
vinavyoshuhudiwa katika baadhi ya nchi za Kiafrika. Zuma amesema, tangu
mwanzoni mwa mwaka huu wa 2014 raia wasio na hatia katika nchi za
Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nigeria, Sudan Kusini na nyinginezo za Afrika
wamelengwa na mashambulizi ya makundi ya kigaidi.
Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika sambamba na kutaka mauaji hayo yakomeshwe, ametoa wito kwa nchi za Kiafrika kufanya jitihada zaidi za kuimarisha amani na usalama kwenye bara hilo. Pia amesisitiza ulazima wa kuanzishwa taasisi za kijamii na kiuchumi kwa ajili ya kudhamini utoaji mishahara, maendeleo na kutayarisha mazingira ya kuwepo tamaduni na dini mbalimbali ili kupatikane amani ya kudumu kwenye bara hilo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!