Ripoti mpya imeonesha kuwa mwanamke mmoja kati ya watatu
katika nchi za Umoja wa Ulaya ameshawahi kushambuliwa au kubwakwa katika
maisha yake.
Ripoti hiyo kuhusiana na kunyanyaswa wanawake iliyolewa na
Taasisi ya Haki za Msingi ya EU (FRA) imeonesha kwamba, asilimia 33 ya
wanawake wanaoshi katika nchi 28 zinazounda Umoja wa Ulaya sawa na watu
milioni 66, wameshawahi kunyanyashwa kijinsia katika maisha yao.
Morten Kjaerum mkuu wa taasisi hiyo amesema, ripoti hiyo
inadhihirisha unyanyasaji mkubwa wanaofanyiwa wanawake lakini
hauripotiwi kwa vyombo husika. Nchi za Derman, Finland na Sweden
zimetajwa kuwa ni nchi ambazo wanawake hunyanyaswa zaidi zikiliganishwa
na nchi nyingine za bara Ulaya.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!