Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria
cha APC kimemkosoa Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo kutokana ufisadi
serikalini na kuwataka wananchi wahitimishe utawala wa miaka 15 wa chama
tawala katika uchaguzi wa mwaka ujao. Chama hicho kimefanya mkutano
wake wa kwanza wa kitaifa tangu kilipoundwa baada ya kuungana vyama
vinne vya siasa miezi 11 iliyopita na kuahidi kuwa iwapo kitashinda
uchaguzi kitapambana na ufisadi, machafuko na kuleta fursa zaidi za
ajira.
Kiongozi wa chama hicho kipya Muhammad
Buhari mtawala wa zamani wa kijeshi na gavana wa zamani amezindua nembo
ya chama hicho kipya na kusema kuwa chama hicho ni kwa ajili ya Nigeria
mpya. Muungano huo wa upinzani unatarajiwa kuleta changamoto kali kwa
chama tawala cha PDP anachotoka Rais Jonathan katika uchaguzi ujao wa
rais ambacho wanachama wake wengi wamekiasi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!