Chama cha upinzani nchini Bahrain
cha al Wifaq kimeitaka jamii ya kimataifa ifanye juhudi za kuzuia mateso
wanayofanyiwa raia nchini humo. Al Wifaq imesema kuwa, baada ya kutokea
mlipuko kwenye eneo la al Salaabas magharibi mwa mji mkuu Mnama ambapo
askari polisi watatu waliuawa, askari wa utawala wa Aal Khalifa
wamegeuza eneo hilo kituo cha kijeshi na kuwakamata vijana wengi wa
Bahrain. Chama hicho kimeitaka jamii ya kimataifa kufanya jitihada za
kukomesha ukiukwaji haki za binadamu nchini Bahrain na kueleza kuwa,
askari wa utawala wa kifalme hivi sasa wanawaadhibu kwa umati wakaazi wa
eneo la al Salaabas kwa kuwashambulia raia, kuvamia nyumba na kuweka
sheria ya kutotoka nje.
Jumuiya ya Kitaifa ya Kidemokrasia ya
Bahrain pia imelaani mashambulizi ya vikosi vya al Khalifa dhidi ya raia
na kusema kuwa ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu. Vituo vya
kutetea haki za binadamu vya Bahrain pia vimetangaza kuwa, watawala wa
nchi hiyo wanatumia vibaya askari usalama na kuzidisha siasa zao za
ukandamizaji hivyo kuna udharura wa jamii ya kimataifa kukomesha suala
hilo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!