Nchi zinazoshiriki mkutano wa
kimataifa kuhusiana na Libya zimepaza sauti zao na kusema kuwa zinatiwa
hofu na kuendelea ukosefu wa usalama na pia kutokuwepo mfumo wa kisiasa
nchini humo. Katika mkutano huo uliofanyika mji mkuu wa Italia, Rome
wawakilishi wa zaidi ya nchi 40 duniani wamesema kuwa, matatizo
yanayoendelea nchini Libya yanaweza kuwa makubwa iwapo hakutopatikana
suluhisho la kisiasa.
Muhammad Abdulaziz Waziri wa Mambo ya
Nje wa Libya ambaye ameshiriki katika mkutano huo ameeleza matatizo
mbalimbali yanayozuia kuwepo hali nzuri ya kisiasa na kiusalama nchini
mwake. Amesema kuwa, Libya ilitekwa nyara kwa zaidi ya miaka 40 huku
vyama vya siasa vikipigwa marufuku.
Mapigano kati ya vikosi vya serikali na
makundi yenye silaha yamepelekea kukosekana amani na usalama wa kudumu
nchini Libya. Makundi hayo ya wanamgambo yalikuwa na nafasi muhimu
katika harakati za mapinduzi yaliyoupindua utawala wa dikteta Muamar
Gaddafi mwaka 2011.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!