Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi UNHCR limesema kuwa, Waislamu wamefukuzwa huko magharibi mwa
Jamhuri ya Afrika ya Kati na maelfu ya raia wanakabiliwa na hatari ya
kuuawa. Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres ameliambia Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa hapo jana kuwa, maelfu ya Waislamu wameikimbia nchi
hiyo huku machafuko kati ya Waislamu na Wakristo yakiendelea. Ameongeza
kuwa, wiki iliyopita pekee Waislamu 15,000 walikuwa wamezingirwa katika
maeneo 18 ya magharibi mwa Jamahuri ya Afrika ya Kati.
Katika upande mwingine Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kupelekwa wanajeshi na polisi
12,000 katika nchi hiyo ya Kiafrika ili kudhibiti hali ya mambo.
Inakadiriwa kuwa, zaidi ya watu 2,000 wameuawa na zaidi ya milioni moja
kukimbia makaazi yao kutokana na machafuko hayo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!