Member wa kundi la Wakacha, Jux ambaye wiki hii ameachia wimbo
alioupa jina la ‘Nitasubiri’ ambao tangu aweke wazi jina la wimbo huo
wengi walianza kuhisi kuwa amemuimbia mpenzi wake Jackie Cliff, ameweka
wazi chanzo cha kuandika wimbo huo.
Jux ameviambia vya habari kuwa hakuuandika wimbo huo kwa maana
ya kuu-dedicate kwa Jackie Cliff, lakini ukweli ni kwamba hizo ndizo
hisia alizokuwa nazo wakati anaandika wimbo huo na ilikuwa ni baada ya
mpenzi wake huyo kupata matatizo nchini China.
“Ni kweli, sijadedicate kabisa kusema nini lakini kipindi ambacho nimerudi ilikuwa hayo mambo yameshatokea na vitu kama hivyo, kwa hiyo nilivyorudi nilikuwa na hiyo idea. Kwa hivyo naweza kusema ilikuwa hivyo kweli.” Jux amesema.
“Kweli kwa kipindi hicho ambacho nimerekodi hiyo nyimbo nilikuwa na feeling hiyo kichwani kwangu na kweli hayo matatizo yalikuwa yameshatokea kama ilivyotokea halafu nikarekodi hiyo nyimbo. Yaani naweza kusema hivyo kwa sababu ndio feeling ambayo nilikuwa nayo kwa huo muda na kitu kilikuwa ndio kishatokea hicho.” Ameongeza.
Ameeleza kuwa ingawa producer wa wimbo huo alimtaka afanye wimbo wa
kuchezeka, yeye aliomba afanye kile anachokifeel kwa muda huo kwa kuwa
nyimbo zake huandika kutokana na hisia za kweli alizonazo, lakini pia
aliona huo ni wimbo wa tofauti sana kwake.
“Hapo kitu ambacho najaribu kusema sikuwahi kusema kwamba naimba hii nyimbo kwa ajili ya mtu fulani, no. Niliingia studio nikamkuta Bob, Bob akaniambia inabidi tufanye nyimbo. Tena Bob alitaka tufanye nyimbo ya kuchezeka. Nikamwambia Bob kitu ambacho kiko kichwani kwangu sasa hivi ambacho kikatoka kitu kizuri. Bob akaniambia yeah...nikamwambia hiki kitu mimi nakiona na inabidi niimbe kitu hiki. Bob akaniambia au unamuimbia nanii, nikamwabia yeah...inaweza ikawa hivyo kwa sababu, ndio kitu ambacho nafeel right now."
Jux na mpenzi wake Jackie Cliff |
“Ni kweli, sijadedicate kabisa kusema nini lakini kipindi ambacho nimerudi ilikuwa hayo mambo yameshatokea na vitu kama hivyo, kwa hiyo nilivyorudi nilikuwa na hiyo idea. Kwa hivyo naweza kusema ilikuwa hivyo kweli.” Jux amesema.
“Kweli kwa kipindi hicho ambacho nimerekodi hiyo nyimbo nilikuwa na feeling hiyo kichwani kwangu na kweli hayo matatizo yalikuwa yameshatokea kama ilivyotokea halafu nikarekodi hiyo nyimbo. Yaani naweza kusema hivyo kwa sababu ndio feeling ambayo nilikuwa nayo kwa huo muda na kitu kilikuwa ndio kishatokea hicho.” Ameongeza.
Jackie Cliff |
“Hapo kitu ambacho najaribu kusema sikuwahi kusema kwamba naimba hii nyimbo kwa ajili ya mtu fulani, no. Niliingia studio nikamkuta Bob, Bob akaniambia inabidi tufanye nyimbo. Tena Bob alitaka tufanye nyimbo ya kuchezeka. Nikamwambia Bob kitu ambacho kiko kichwani kwangu sasa hivi ambacho kikatoka kitu kizuri. Bob akaniambia yeah...nikamwambia hiki kitu mimi nakiona na inabidi niimbe kitu hiki. Bob akaniambia au unamuimbia nanii, nikamwabia yeah...inaweza ikawa hivyo kwa sababu, ndio kitu ambacho nafeel right now."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!