Klabu ya Barcelona imekatiza matumaini ya Manchester City katika
michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mara baada ya kuifunga kwa
goli 2-1 pale Nou Camp na kutinga robo fainali kwa ushindi wa jumla ya
magoli 4-1.
Lionel Messi aliiweka Barcelona katika hali nzuri mara baada ya kufunga goli la kuongoza katika kipindi cha pili na kuivunja nguvu Man City iliyokuwa ikihitaji kusawazisha kufuatia kufungwa goli 2-0 katika mchezo wa kwanza wa Etihad Stadium.
Beki wa Man City,Pablo Zabaleta alitolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kupewa njano ya pili kutokana kumlalamikia mwamuzi kwa kushindwa kuwazawadia penati.
Vincent Kompany aliifungia Man City goli katika dakika za mwisho
wakati wakiwa pungufu lakini bado kulikuwa na muda kwa Dani Alves
kufunga goli la ushindi kwenye sekunde za mwishoni kabisa na kuifanya
Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Man City walikuwa na bahati licha ya kuanza mchezo vizuri kufuatia
mwamuzi,Stephane Lannoy kutowapa adhabu ya penati mara baada ya Joleon
Lescott kumchezea faulo Messi katika eneo la hatari ikiwa ni dakika ya
tisa ya mchezo.
Vijana hao wa Manuel Pellegrini walipoteza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa James Milner na David Silva huku meneja wao huyo raia wa Chile akishuhudia mpambano akiwa jukwaani kutokana na kutumikia adhabu aliyopewa na UEFA kwa kosa la kumkosoa mwamuzi wa mchezo wa kwanza uliopigwa Etihad.
Pia wangeweza kupata penati dakika 12 kabla ya mpira kuisha mara
baada Edin Dzeko kufanyiwa faulo na Gerard Pique katika eneo la hatari
ila mwamuzi hakuweza kutoa adhabu yeyote kwa wenyeji hao.
Kabla ya Zabaleta kutolewa nje aliweza kukosa nafasi ya kufunga kufuatia kupata klosi safi kutoka kwa Aleksandar Kolarov.
Lionel Messi aliiweka Barcelona katika hali nzuri mara baada ya kufunga goli la kuongoza katika kipindi cha pili na kuivunja nguvu Man City iliyokuwa ikihitaji kusawazisha kufuatia kufungwa goli 2-0 katika mchezo wa kwanza wa Etihad Stadium.
Beki wa Man City,Pablo Zabaleta alitolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kupewa njano ya pili kutokana kumlalamikia mwamuzi kwa kushindwa kuwazawadia penati.
Vijana hao wa Manuel Pellegrini walipoteza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa James Milner na David Silva huku meneja wao huyo raia wa Chile akishuhudia mpambano akiwa jukwaani kutokana na kutumikia adhabu aliyopewa na UEFA kwa kosa la kumkosoa mwamuzi wa mchezo wa kwanza uliopigwa Etihad.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!