Beki wa Manchester City,Pablo Zabaleta
amemtuhumu mwamuzi kutoka Ufaransa,Stephane Lannoy kwa maamuzi yake ya
kushtusha dhidi yake katika mchezo waliofungwa 2-1 na Barcelona.
Raia huyo wa Argentina,alitolewa nje katika
uwanja wa Nou Camp kufuatia kupewa kadi mbili za njano,huku kadi ya pili
ikionyeshwa mara baada ya kumzonga Lannoy kuhoji kwanini alishindwa
kutoa adhabu ya penati kufuatia Edin Dzeko kufanyiwa faulo na Gerard
Pique kwenye eneo la hatari.
Barcelona pia walistahili kupewa penati halali
wakati Messi alipoangeshwa katika eneo la hatari na Lescott katika
kipindi cha kwanza huku wakinyimwa pia goli kwa madai walikuwa wameotea
wakati marudio ya picha za video zilionyesha wazi kuwa Jordi Alba
alikuwa eneo sahihi wakati akitoa klosi kwa Neymar ambaye aliukwamisha
mpira wavuni.
Zabaleta alikuwa anaamini Man City walistahili
kupewa penati kwa madhambi aliyofanyiwa Dzeko na anadai kuwa yupo
gizani kwa kutokufahamu kwanini alitolewa nje na mwamuzi.
Huku akisisitiza,”Ilikuwa wazi sana.Nafikiri
Pique alikuwa nyuma yangu na alifanya ukabaji mbaya kwa Dzeko na
kumwangusha chini huku mwamuzi akiwa mita mbili kutoka mahali
lilipotokea tukio hilo.”
Na kuongeza kuwa,”Sifahamu kwanini nilitolewa nje.Nilienda kwake kuongea naye kwa njia ya utaratibu kabisa.”
Pia akakiri kuwa alikuwa na hasira sana kwa mwamuzi huyo kwasababu hakuwapa penati lakini mara zote maekuwa akimuheshimu sana.
Lakini alisisitiza kuwa ameumizwa na
kusikitishwa sana kwani anafikiri ulikuwa uwamuzi wa kushtusha
sana.Akiongeza kuwa mara nyingine katika mchezo wanakuwa na wasiwasi na
presha kwasababu wanakuwa wanajaribu kupata matokeo mazuri na maamuzi
mabaya ya refa huwapa hasira sana.
Zabaleta akaongeza kuwa anahisi Man City
walistahili kupewa faulo kutokana na Dzeko kufanyiwa faulo sekunde
chache kabla ya Messi kufunga goli.
Mwisho akathibitisha hasira zake na masikitiko
yake lakini akatoa pongezi kwa timu yake kwasababu anafikiri walicheza
mpira wa kiwango cha juu sana kwani walianza mchezo vizuri na kumaliza
vizuri na walikuwa na uwezo wa kufunga mwanzo na walikuwa na nafasi
nyingine kadhaa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!