Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wameelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati
kwa shabaha ya kuanza uchunguzi wa kina juu ya vitendo vya ukiukwaji wa
haki za binadamu uliofanywa nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa timu ya watu watatu ya wakaguzi wa Umoja wa Mataifa itabaki nchini humo kwa muda wa wiki mbili na kuzungumza na wahanga na mashuhuda wa matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Imeelezwa kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwa wale watakaobainika kuhusika na mauaji na vitendo vingine vya kikatili, kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliyoko Uholanzi. Bernard Acho Muna mkuu wa Kamisheni ya Kimataifa ya Uchunguzi iliyoundwa mwezi Januari na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon, amesema kuwa jukumu la timu hiyo ni kuzuia kutokea mauaji ya kimbari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, kundi la Kikristo la Anti Balaka limekuwa likifanya vitendo vya mauaji, ubakaji, kuharibu na kuchoma moto Misikiti na nyumba za Waislamu na hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui. Machafuko nchini humo yamepelekea maelfu ya watu kuuawa na karibu robo moja ya watu milioni nne na laki sita wa nchi hiyo wamelazimika kuwa wakimbizi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!