Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SOMA KILE ILICHO KISEMA SERIKALI YA SOMALIA KWA KUNDI LA KIISLAM LA AL-SHAABAB

SOMA KILE ILICHO KISEMA SERIKALI YA SOMALIA KWA KUNDI LA KIISLAM LA AL-SHAABAB

Written By Unknown on Tuesday, 11 March 2014 | Tuesday, March 11, 2014

Serikali ya Somalia imetangaza kuwa iko tayari kuwasamehe wapiganaji wa kundi la al Shabab mkabala wa kundi hilo kuweka chini silaha zao.
Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Sheikh Ahmed ameyasema hayo baada ya kuanza operesheni kamambe ya kijeshi inayolishirikisha jeshi la taifa la Somalia na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM kwenye maeneo matatu ya katikati na kusini mwa nchi hiyo. Waziri Mkuu wa Somalia ameongeza kuwa, vikosi vya jeshi la AMISOM na majeshi ya Somalia kwa pamoja yamefanikiwa kukomboa miji mitano ya kiistratijia iliyoko kusini magharibi mwa nchi hiyo ukiwemo mji wa Bakol ambao kwa miaka kadhaa ulikuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo wa al Shabab.
Kundi la al Shabaab limekuwa likipoteza udhibiti wake katika maeneo mengi ya kusini na katikati mwa Somalia tangu mwaka 2011.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi