Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BADO SAUDI ARABIA YASISITIZA KUKATA UHUSIANO NA QATAR

BADO SAUDI ARABIA YASISITIZA KUKATA UHUSIANO NA QATAR

Written By Unknown on Tuesday, 11 March 2014 | Tuesday, March 11, 2014

Serikali ya Saudi Arabia imekataa upatanishi wa aina yoyote wenye shabaha ya kutatua mgogoro ulioko kati ya nchi hiyo na Qatar.
Taarifa zinasema kuwa, Saudi Arabia imekataa juhudi za upatanishi za baadhi ya nchi za Magharibi na za Kiarabu zenye shabaha ya kurejeshwa uhusiano kati ya serikali za Riyadh na Doha.
Siku ya Jumatano iliyopita, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain ziliwarejesha nyumbani mabalozi wao waliokuwa Doha baada ya nchi hizo kuituhumu Qatar kwamba inakwenda kinyume na misingi ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.

Kwa upande wake serikali ya Qatar imesema kuwa, maamuzi hayo hayatakuwa na maslahi yoyote kwa nchi za eneo hilo bali yatasababisha kukosekana amani na utulivu. Taarifa ya serikali ya Qatar imeeleza kuwa, nchi hiyo haiko tayari kubadilisha siasa zake za kigeni kwa lengo la kuzifurahisha nchi nyingine. Msimamo huo wa Qatar una mwelekeo wa kuendelea na siasa zake za kuiunga mkono kikamilifu harakati ya Ikhwanul Muslimiin nchini Misri.
Mgogoro kati ya nchi hizo unatokana na msimamo wa Qatar wa kuiunga mkono kikamilifu harakati ya Ikhwanul Muslimiin ya Misri, huku nchi hizo zikiiunga mkono serikali ya mpito ya Misri ambayo inadai kuwa Ikhwanul Muslimiin ni kundi la kigaidi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi