Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » LEO KATIKA HISTORIA

LEO KATIKA HISTORIA

Written By Unknown on Tuesday, 11 March 2014 | Tuesday, March 11, 2014

Siku kama ya leo mwaka 1110 kisiwa cha Malta maarufu kama "Herini ya Mediterania" kilitwaliwa na Waislamu na kuunganishwa na mamlaka ya nchi za Kiislamu. Utawala wa Waislamu wa kisiwa cha Malta uliendelea hadi mwaka 1091 yaani hadi zama za udhibiti wa kaumu ya Norman kisiwani humo.
Malta ambayo inaundwa na visiwa vingi vidogo na vikubwa ina ukubwa wa kilomita mraba 316 na jamii ya watu karibu nusu milioni.

 ***********************************************************

Tarehe 9 Jamadil Awwal mwaka 786 Hijria, aliuawa shahidi faqihi na mtaalamu mkubwa wa hadithi Muhammad bin Jamaluddin Makki Amili, mashuhuri kwa jina la "Shahidi wa Kwanza." Alizaliwa mwaka 734 Hijria katika mojawapo ya vijiji vya Jabal Amil nchini Lebanon. Alijifunza elimu mbalimbali kutoka kwa walimu wakubwa wa zama zake kama vile Allama Hilli. Mbali na elimu ya dini, Muhammad bin Jamaluddin pia alikuwa hodari katika taaluma za mashairi na fasihi. Katika miaka 52 ya umri wake uliojaa baraka, Shahidi wa Kwanza aliandika vitabu vingi, ikiwa ni pamoja na "Albaqiyatus-Swalihat" na "al Lumuatu Dimashqiyya." Aliuawa na wapinzani wenye taasubi katika siku kama ya leo.

 ***********************************************************

Na tarehe 11 Machi miaka 10 iliyopita milipuko mitano ya bomu iliyotokea katika vituo kadhaa vya treni ya chini ya ardhi mjini Madrid, Uhispania ilisababisha vifo vya karibu watu 200 na kujeruhi wengine elfu moja. Milipuko hiyo inahesabiwa kuwa operesheni kubwa zaidi ya kigaidi barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Japokuwa serikali ya mrengo wa kulia ya wakati huo ya Uhispania ililituhumu kundi la waasi wa ETA kuwa ndilo lililotekeleza mashambulizi hayo, lakini kundi la al Qaida lilitoa taarifa likitangaza kuwa ndilo lililohusika na milipuko hiyo.
Moja ya matokeo ya mashambulizi ya tarehe 11 Machi mjini Madrid ilikuwa kushindwa chama cha kisoshalisti katika uchaguzi wa Bunge na kuondolewa askari wa Uhispania nchini Iraq.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi